Home Sports SIMBA WAANZA KAZI KUKAMILISHA MECHI MBILI

SIMBA WAANZA KAZI KUKAMILISHA MECHI MBILI

MECHI mbili zimebaki kwa Simba kukamilisha ndani ya msimu wa 2022/23 ikiwa ni dakika 180.

Simba ipo nafasi ya pili kwenye msimamo na vinara wa ligi ni Yanga ambao wametwaa ubingwa wa ligi msimu huu.

Ikumbukwe kwamba Yanga inaiwakilisha Tanzania kwenye anga za kimataifa ikiwa ipo hatua ya fainali Kombe la Shirikisho Afrika na itapambana na USM Alger Juni 3.

Kikosi hicho chini ya Kocha Mkuu, Roberto Oliveira kimeanza maandalizi kwa mechi hizo.

Ni dhidi ya Polisi Tanzania unaotarajiwa kuchezwa Juni 6 na ile kete ya pili na ya mwisho inatarajiwa kuchezwa Juni 9.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari ndani ya Simba amesema wapo tayari kwa mechi hizo mbili.

“Tunahitaji kufanya vizuri kwenye mechi zetu ambazo zimebaki na tunajua kutakuwa na ushindani mkubwa mashabiki wajitokeze kwa wingi,”.

Miongoni mwa nyota ambao wameanza mazoezi ni pamoja na Onyango Joash, Henock Inonga, John Bocco, Jean Baleke.

Previous articleMUDA WA YANGA KUREJESHA TABASAMU KWA WANANCHI
Next articleVIDEO:RICARDO MOMO AFUNGUKIA KUCHEZA YANGA