Home International NGOMA NZITO UEFA

NGOMA NZITO UEFA

NGOMA imekuwa ngumu kwa wababe wote wawili kusepa na ushindi katika mchezo wa UEFA Champions League.

Ubao wa Uwanja wa Santiago Bernabeu umesoma Real Madrid 1-1 Manchester City ikiwa ni hatua ya nusu fainali ya Kwanza.

Vini Jr alianza kutupia upande wa Real Madrid dakika ya 36 kipindi cha kwanza bao ambalo lilisawazishwa kipindi cha pili.

Ni Kevin De Bruyne mwamba aliweka usawa dakika ya 67 na kufanya ngoma kuwa sawa Kwa wote.

Real Madrid ilipiga mashuti 13 ni manne yalilenga lango na Manchester City ilipiga mashuti 10 na ni sita yalilenga lango.

Previous articleKIUNGO MGUMU SIMBA LAZIMA ABADILIKE
Next articleMWAMBA HUYU MBEYA CITY MKALI WA NYAVU