Home Uncategorized MWAMBA HUYU MBEYA CITY MKALI WA NYAVU

MWAMBA HUYU MBEYA CITY MKALI WA NYAVU

UKIFIKA Mbeya usisahu ukarimu wa watu wale na namna wanavyojivunia uoto wa asili hakika kàtika hili wanastahili pongezi.

Wanasema kàtika orodha ya marafiki ulionao usisahau kuwa na mmoja anayetoka Mbeya hakika hautajuta ni furaha muda wote kuwa na rafiki kutoka nyanda za juu kusini.

Hata Deus Kaseke anayekipiga ndani ya Singida Big Stars ni zao la Mbeya anajivunia kutoka huko pia.

Ipo wazi kuwa Tanzania ni amani na Upendo hivyo ukarimu sio Mbeya pekee kila Kona Hali hiyo ipo.

Tukirudi uwanjani kuna Mbeya City yenye Sixtus Sabilo ambaye kihalisia ni kiungo mshambuliaji lakini ni mzuri kwenye kufunga.

Mabao kibindoni ni 9 ametoa pasi sita mzawa huyu akihusika kwenye jumla ya mabao 15 Kati ya 30 yaliyofungwa na timu hiyo.

Timu hiyo inapambana kujiokoa kwenye hatari ya kushuka daraja kutokana na mwendo wake kuwa wa kusuasua kwenye ligi.

Ipo nafasi ya 13 Mbeya City kibindoni ina pointi 27 ina mechi tatu mkononi ambazo ikifanya vibaya nafasi yake pia itakuwa mbaya.

Ni muda wa lala salama na kila mchezaji kutimiza wajibu wake kwenye msako wa pointi tatu muhimu.

Previous articleNGOMA NZITO UEFA
Next articleNAHODHA SIMBA AOMBA RADHI KWA MASHABIKI