JOHN Bocco nahodha wa Simba amesema kuwa matokeo ambayo wameyapata hawajapenda lakini ni mpira jambo waliomba radhi kwa mashabiki.
Simba imepoteza nguvu ya kutwaa taji lolote msimu wa 2022/23 baada ya matumaini yao kuzimika kwenye kila idara.
Katika ligi wapo nafasi ya pili huku vinara wakiwa ni Yanga wanaohitaji pointi tatu watetee ubingwa wao, katika kombe la Azam Sports Federation wameondolewa hatua ya nusu fainali.
Pia kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika wamegotea hatua ya robo fainali wakishindwa kutimiza malengo ya kutinga hatua ya nusu fainali.
Bocco amesema:”Tunawaomba radhi mashabiki kwa kushindwa kufikia malengo ya kutwaa taji lolote msimu huu tutatumia mechi zilizobaki kujipanga kwa wakati ujao,”.
Mchezo ujao kwa Simba ni dhidi ya Ruvu Shooting unaotarajiwa kuchezwa Ijumaa, Uwanja wa Azam Complex.
Tottenham Hotspur forward Dominic Solanke battles with Crystal Palace defender Maxence Lacroix during the English championship Premier League football match between Crystal Palace and Tottenham Hotspur on 27 October 2024 at Selhurst Park in London, England - Photo Ian Stephen / ProSportsImages / DPPI (Photo by IAN STEPHEN / ProSportsImages / DPPI via AFP)