KIUNGO MGUMU SIMBA LAZIMA ABADILIKE

    KIUNGO Kanoute lazima akubali kubadilika kutokana na mikato yake ya kimyakimya kuigharimu timu yake kila mara.

    Miongoni mwa wachezaji imara na bora wawapo uwanjani kwenye eneo la ukabaji huwezi kumuweka kando Sadio Kanoute.

    Huyu ni kiungo wa ukabaji asilia lakini amekuwa akiigharimu mara nyingi timu pamoja na kutokuwa mlinzi mzuri kwa wachezaji wa timu pinzani.

    Mtindo wa n’ge na viwiko vile vya kimyakimya amekuwa akitumia na ikumbukwe kwamba aliwahi kukutana na kiungo wa Yanga Khalid Aucho kwenye Dabi.

    Mkato aliotemezewa ulimfanya akae nje ya uwanja kwa muda akipambania afya yake hivyo ni lazima awe mlinzi kwa wengine katika mechi anazocheza.

    Ni nyota anayeongoza kuonyeshwa kadi nyekundu ndani ya kikosi cha Simba na zote zinatokana na kadi mbili za njano.

    Ilikuwa mchezo wa ligi dhidi ya Coastal Union pale Tanga alionyeshwa kadi mbili za njano na Jonesia Rukya kisha mchezo wa pili ni dhidi ya Azam FC.

    Wakati timu inasaka ushindi alifunga bao moja la usawa kisha akacheza faulo zaidi ya mbili na kuonyeshwa kadi mbili za njano.

    Dakika ya 85 timu ya Simba imetunguliwa mabao mawili inafungwa bao lingine kwa kumkosa kiungo wa kazi ngumu Kanoute aliyekuwa kwenye mikono ya James Akamiko.

    Licha ya kwamba na yeye alichezewa faulo haina maana ni lazima alipe kisasi kwa makusudi hapana, mchezaji mkubwa haonyeshwi kadi ya njano kwenye mchezo mkubwa.

    Hata kwenye mashindano ya kimataifa kuna mechi alikosekana kutokana na kadi za njano hili lazima alifanyie kazi kubwa bora zaidi.

    Mikato ya kimyakimya ni sumu kwa mchezaji mkubwa lazima abadilike kuwa bora zaidi na kutimiza majukumu yake

    Previous articleKIBOKO YA AIR MANULA NI MOTO WA KUOTEA MBALI
    Next articleNGOMA NZITO UEFA