Home Sports KIBOKO YA AIR MANULA NI MOTO WA KUOTEA MBALI

KIBOKO YA AIR MANULA NI MOTO WA KUOTEA MBALI

MTAMBO wa mabao ndani ya Azam FC, Prince Dube kahusika kwenye mabao 10 ndani ya timu hiyo inayonolewa na Kali Ongala.

Dube kampa tabu pia kipa namba moja wa Simba, Aishi Manula kwa kumtibulia rekodi zake za kutofungwa kwenye mechi zote mbili za ligi walipokutana Uwanja wa Mkapa.

Manula wa Simba ni namba mbili kwa makipa ambao hawajafungwa kwenye mechi mbili nama moja ni Djigui Diarra wa Yanga.

Katika mchezo wa kwanza Dube alimtungua Manula Azam iliposepa na pointi tatu mazima na mchezo wapili Azam FC ilitoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1.

Nyota huyo ambaye kasi yake imekuwa ni ya kusuasua kutokana na kuanza msimu akisumbuliwa na majeraha bado kaonesha balaa lake kwenye mechi anazocheza.

Mechi 18 kacheza ndani ya Ligi Kuu Bara ambazo alianza kikosi cha kwanza akiwa ametupia mabao sita na pasi zake ni nne za mabao huku akiwa ni chaguo la kwanza la Ongala pale anapokuwa fiti.

Azam FC imefunga jumla ya mabao 44 ikiwa nafasi ya tatu kwenye msimamo na imekusanya pointi 53 kibindoni.

Ongala amesema kuwa kila siku wanafanyia kazi makosa kwenye kila idara ili kufunga mabao mengi zaidi.

“Kwenye mechi ili ushinde lazima upate mabao mengi na tumekuwa tikiboresha makosa ili kuongeza uimara kwenye safu ya ushambuliaji pamoja na ulinzi,”.

Pia Dube alimtungua kipa namba tatu wa Simba, Ally Salim kwenye mchezo wa hatua ya nusu fainali ya Azam Sports Federation.

Previous articleHAWATAAMINI WASAUZI,SIMBA YAMALIZANA NA STRAIKA WA MABAO
Next articleKIUNGO MGUMU SIMBA LAZIMA ABADILIKE