Home International ISHU YA FEISAL TFF HUKUMU IMEGOTEA HAPA

ISHU YA FEISAL TFF HUKUMU IMEGOTEA HAPA

KAMATI ya Sheria na Hadhi za Wachezaji la Shirikisho la MPIRA wa Miguu Tanzania,(TFF) limetupilia mbali maombi ya Feisal Salum kuhusu kesi yake na Yanga.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisa Habari wa TFF, Clifford Ndimbo imeeleza kuwa Mei 4,2023 pamoja na mambo mengine lilisikiliza shauri la mchezàji Feisal Salum aliyewasilisha malalamiko akitaka kuvunja mkataba wake na Yanga.

Hayo yote yalielezwa kupitia barua yake ya Machi 6,2023.

Awali Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ilisikiliza malalamiko hayo Kwa njia ya maandishi ambapo pande zote Yanga na Feisal ziliwakilishwa na wanasheria wao ambao walipewa pia muda wa nyongeza wa kufafanua walichowasilisha kwenye majumuisho yao ya maandishi.

Baada ya kupitia na kutafakari kwa kina hoja zote za pande husika, Kamati imetupilia mbali maombi hayo kwa msingi kwamba ilishaamua juu ya uhalali wa mkataba wa mchezàji huyo na klabu yake kwamba ana mkataba unaoendelea mpaka 2024.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa suala la kuvuja mkataba na timu kanuni inaeleza mchezaji ni lazima aanze majadiliano na klabu husika ambayo ina haki katika suala hilo.

Previous articleVIDEO:ISHU YA SARE NAMUNGO SIMBA WACHARUKA
Next articleSIMBA KAMILI KUIKABILI AZAM FC