Home Sports SIMBA KAMILI KUIKABILI AZAM FC

SIMBA KAMILI KUIKABILI AZAM FC

UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa upo tayari kwa ajili ya mchezo wao ujao dhidi ya Azam FC.

Mshindi wa mchezo huo atakutana na mshindi kati ya Singida Big Stars v Yanga mchezo unaotarajiwa kupangiwa tarehe kutokana na Yanga kuwa na kazi ya kusaka ushindi mchezo wa nusu fainali Kombe la Shirikisho Afrika.

Ni Mei 7 mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Nangwanda, Sijaona ikiwa ni hatua ya nusu fainali kombe la Azam Sports Federation.

Simba imetoka kugawana pointi moja na Namungo, Uwanja wa Majaliwa kwa kufungana bao 1-1 inakwenda kumenyana na Azam FC iliyotoka kushinda mabao 3-1 dhidi ya Ruvu Shooting.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo na wanachukua tahadhari zote kuwakabili Azam FC.

“Tunatambua mchezo wetu utakuwa mgumu lakini tupo tayari tunahitaji kupata ushindi kwenye mchezo huo ili tusonge mbele hatua ya fainali,”.

Kikos hicho leo kimeibukia Mtwara kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo huo na miongoni mwa wachezaji waliopo kwenye msafara huo ni Mzamiru Yassin, Pape Sakho, Shomari Kapombe.

Previous articleISHU YA FEISAL TFF HUKUMU IMEGOTEA HAPA
Next articleWAKALI WAKIWA LANGONI HAWA HAPA