Home Uncategorized YANGA HAO NUSU FAINALI KIMATAIFA CAF

YANGA HAO NUSU FAINALI KIMATAIFA CAF

YANGA inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi imeandika historia bora ya kutinga hatua ya nusu fainali Kombe la Shirikisho Afrika.

Faida ya mabao ya ugenini ubao uliposoma Rivers United 0-2 Yanga umewapa nguvu kusonga mbele.

Mabao yote yalifungwa na Fiston Mayele akitumia pasi za Bakari Mwamnyeto.

Katika mchezo wa leo Uwanja wa Mkapa wametoshana nguvu bila kufungana hivyo Yanga anapita jumlajumla.

Ni Gallats atakutana nao ambao wameshinda dhidi ya Pryamids Kwa jumla ya mabao 2-1.

Kuanzia kipindi cha kwaza Yanga walicheza kwa nidhamu huku wakitengeneza mashambulizi kupitia kwa Mudhathir Yahya, Mayele, Aziz KI.

Jesus Moloko aliingia kipindi cha pili na kuongeza nguvu ya kumwaga majalo lakini hayakuleta matunda kwenye mchezo wa leo.

Previous articleLIVERPOOL YASHINDA USIKU KWELI
Next articleSISI NDIO YANGAAA, SIMBA YACHORA RAMANI KUIVURUGIA YANGA