Home Uncategorized SIMBA YAWATUNGUA YANGA KWA MKAPA

SIMBA YAWATUNGUA YANGA KWA MKAPA

SIMBA imepata ushindi mbele ya Yanga kwenye mchezo wa Kariakoo ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Mabao ya Simba yamefungwa na Henock Inonga dakika ya kwanza na lile la pili Kibu Dennis dakika ya 33.

Yanga wanapiga pasi nyingi kuliskama lango la Simba huku wakifanya majaribio kupitia kwa Fiston Mayele.

Kipindi cha pili Yanga walirejea kwa kasi kusaka ao huku Simba wakicheza kwa kujilinda zaidi.

Kipa Ally Salim ni nyota wa mchezo akiwa ameyeyusha dakika 90 bila kufungwa mbele ya watani za jadi.

Previous articleJULIO ATOA NENO LA MATUMAINI KMC
Next articleSISI SIO LEVEL ZENU