Home Sports HAALAND NI MASHINE YA MABAO HUKO

HAALAND NI MASHINE YA MABAO HUKO

MSHAMBULIAJI wa Manchester City, Erling Haaland yuko mbioni kufuta kabisa rekodi za ufungaji za Cristiano Ronaldo na Lionel Messi katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Na hivi karibuni anaweza kumpita mpinzani wake mkuu kwa sasa, Kylian Mbappe katika orodha ya wafungaji bora wa muda wote.

Haaland amekuwa mchezaji wa tatu kufunga mabao matano kwenye mechi moja ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, baada ya Messi na mshambuliaji wa zamani wa Shakhtar Donetsk, Luiz Adriano, katika mchezo ambao Man City waliibuka na ushindi wa mabao 7-0 dhidi ya RB Leipzig, Jumatano iliyopita.

Mshambuliaji huyo alikuwa na uwezo wa kufunga mabao zaidi ya hayo lakini alifanyiwa mabadiliko na Kocha Pep Guardiola. Kutokana na jambo hilo Waandishi wa Habari walihoji sababu ya kumtoa, ambapo Pep alijibu:

“Alifunga mabao matano. Tatizo kila tusipofunga mawili au matatu atakosolewa. Huu ndio ukweli,” alisema Pep na kuongeza:

“Hangekuwa na lengo la kufikia siku zijazo. Hapa na kila mahali. Ndio maana nikafanya mabadiliko. Sikujua kuhusu Messi na Leverkusen, lakini nafanya mabadiliko kwa sababu kawaida mchezo unapomalizika tunataka wacheze.”

Namba 9 huyo wa Man City bado ana umri wa miaka 22 tu lakini amewapita baadhi ya washambuliaji mashuhuri akiwemo Wayne Rooney katika michuano hii mikubwa Ulaya.

Ni miaka mitatu na nusu tangu Haaland ajitangaze kwa ulimwengu kwa kufunga hat-trick kipindi cha kwanza katika mechi yake ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa akiwa na Red Bull Salzburg dhidi ya Genk.

Tangu wakati huo hajakata tamaa, amekuwa akiendelea kuwa na wastani mzuri wa kufunga bao kwa kila mchezo tangu akiwa Salzburg, Borussia Dortmund na sasa City.

Kufunga mabao matano kunamfanya afikishe mabao 33 ambayo ni vigumu kuamini katika mechi zake 25 za kwanza kwenye mashindano hayo. Lakini Messi, Ronaldo na Mbappe ukiwalinganisha naye unadhani nani ataonekana mbabe? Endelea kusoma.

Mbappe alianza kucheza akiwa akiwa kijana baada ya kufanya vyema akiwa na Monaco ambao walifanya vyema kwa kutinga hadi nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa 2016-17.

Tangu wakati huo ameshinda Kombe la Dunia, akafunga hat-trick katika fainali ya michuano hiyo, na ndiye mfungaji bora wa muda wote wa PSG.

Lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 bado hajapata taji lake kubwa zaidi katika ngazi ya klabu. Amefunga mabao 40 katika mechi 61 za Ligi ya Mabingwa lakini baada ya kuondolewa katika hatua ya 16 bora msimu huu pengine Haaland anakwenda juu yake katika orodha ya wafungaji msimu huu licha ya kuwa amecheza mechi chache karibia nusu ya alizocheza yeye.

Wachezaji wawili wanaotamba katika zama hizi, Messi na Ronaldo wako mbele kama wafungaji bora wa muda wote wa Uefa, Ronaldo ana mabao 140 na Messi 129. Lakini wanaweza siku moja kuzidiwa.

Hapa tunaangalia rekodi Haaland kwenye Uefa kwa kumlinganisha na Mbappe, Messi na Ronaldo kupitia mechi zao 25 za kwanza kwenye Uefa.

ERLING HAALAND

Mechi: 25

Mabao: 33

Asisti: 3

Bao kwa dakika: 56.5

Bao/asisti kwa dakika: 51.8

Hat-tricks: 2

Penalti: 4

KYLIAN MBAPPE

Mechi: 25

Mabao: 14

Asisti: 8

Bao kwa dakika: 135.3

Bao/asisti kwa dakika: 86.1

Hat-tricks: 0

Penalti: 0

LIONEL MESSI

Mechi: 25

Mabao: 12

Asisti: 6

Bao kwa dakika: 86.4

Bao/asisti kwa dakika: 57.6

Hat-tricks: 0

Penalti: 0

CRISTIANO RONALDO

Mechi: 25

Mabao: 0

Asisti: 7

Bao kwa dakika: Hakuna

Bao/asisti kwa dakika: 270

Hat-tricks: 0

Penalti: 0

ReplyForward

Previous articleANGA LA KIMATAIFA SIMBA NA YANGA ZATESA KWA MKAPA
Next articleMASTAA AZAM FC WAPEWA ONYO