Home Sports ANGA LA KIMATAIFA SIMBA NA YANGA ZATESA KWA MKAPA

ANGA LA KIMATAIFA SIMBA NA YANGA ZATESA KWA MKAPA

KWENYE anga la kimataifa wawakilishi wa Tanzania Simba katika Ligi ya Mabingwa Afrika na Yanga kwenye Kombe la Shirikisho wamefanya kweli kwa kukusanya pointi za kutosha Uwanja wa Mkapa.

Yanga wamekimbiza kwenye kusepa na pointi ambazo ni 9 wakiwa hawajaacha hata moja katika mechi walizocheza Uwanja wa Mkapa huku Simba ikisepa na pointi sita na imeyeyusha pointi tatu.

Jumla kwenye mechi sita za kimataifa yamefungwa mabao 17 ambapo timu za Tanzania zimefungwa mabao manne.

Simba inaongoza kwa kufungwa mabao mengi ambayo ni matatu dhidi ya Raja Casablanca huku Yanga kiwa imefungwa bao moja pekee dhidi ya TP Mazembe.

Kwa upande wa ushindi Yanga imeshinda mechi zote tatu ilizocheza Uwanja wa Mkapa huku Simba ikipoteza mchezo mmoja na kushinda mechi mbili.

Ni mabao 8 Simba imefunga Uwanja wa Mkapa huku Yanga ikifunga jumla ya mabao 7 ambapo kinara wa jumla kwenye utupiaji Uwanja wa Mkapa ni Clatous Chama akiwa amefunga mabao manne na kinara wa kutengeneza pasi ni Kennedy Musonda akiwa ametengeneza pasi tatu yupo zake Yanga.

Mwendo wa Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi upo namna hii:-Yanga 3-1 TP Mazembe, Yanga 2-0 Real Bamako,Yanga 2-0 US Monastir.

Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Roberto Oliveira mwendo wake upo namna hii:-Simba 0-3 Raja Casablanca, Simba 1-0 Vipers, Simba 7-0 Horoya.

 

Previous articleMSAKO WA VIPAJI UWE NA MWENDELEZO
Next articleHAALAND NI MASHINE YA MABAO HUKO