Home Sports MASTAA AZAM FC WAPEWA ONYO

MASTAA AZAM FC WAPEWA ONYO

KALI Ongala, Kocha Mkuu wa Azam FC amesema kuwa amewaambia wachezaji wote wa timu hiyo ni lazima wajitafakari kutokana na matokeo wanayopata na kuonyesha kwa vitendo.

Timu hiyo mchezo wake uliopita ilishuhudia ubao wa Uwanja wa Highland ukisoma Ihefu 1-0 Azam FC jambo lililowafanya waache pointi tatu mazima ugenini.

Imetolewa kwenye mwendo wa kuwania ubingwa wa ligi kutokana na mechi zake tano zilizobaki kuwapa pointi ambazo hazitawakufikia vinara Yanga wenye pointi 65 huku Azam wana pointi 47.

Ongala amesema:”Kilichotokea kwenye mchezo wetu uliopita tulikaa na wachezaji na kuzungumza nao kwani na kuwaambia kwamba wanapaswa wajitafakari kutokana na kile ambacho kinatokeo.

“Lakini muhimu zaidi ni kuwa na mwendo mzuri na kufanya yote kwa vitendo kwani tunaweza kuzungumza siku nzima na tusimalize,”.

Timu hiyo ilikuwa imealikwa kucheza na Gor Mahia ya Kenya Jumapili mchezo wa kirafiki safari hiyo imesitishwa kutokana na sababu za kiusalama.

Previous articleHAALAND NI MASHINE YA MABAO HUKO
Next articleKOCHA SIMBA ANAAMINI VIWANGO VINAZIDI KUPANDA