YANGA 1-0 US MONASTIR

UBAO wa Uwanja wa Mkapa unasoma Yanga 1-0 US Monastri ikiwa ni mchezo wa hatua ya makundi Kombe la Shirikisho.

Yanga wanapambana kusepa na pointi tatu muhimu kujihakikishia nafasi ya kutinga hatua ya robo fainali.

Bao la kuongoza limefungwa na Kenned Musonda kipinda cha kwanza dakika ya 33.

Musonda ametimiza majukumu yake akitumia pasi ya mwamba Jesus Moloko ikiwa kwa sasa ni mapumziko.

Katika mchezo wao walipokutana ugenini Yanga ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-0.