Home Sports MWEDNO WA RUVU NI WA KINYONGA

MWEDNO WA RUVU NI WA KINYONGA

MWENDO wa Ruvu Shooting kwa msimu wa 2022/23 hakika ni wa kinyonga kutokana na kushindwa kuwa kwenye ule ubora wao wa kupapasa.

Kwenye msimamo ipo nafasi ya 15 imekusanya pointi 20 baada ya kucheza mechi 25.

Ukuta wao umeruhusu kutunguliwa mabao 30 huku ile safu yao ya ushambuliaji ikitupia mabao 16.

Timu hiyo imepoteza jumla ya mechi 15 na ushindi ni kwenye mechi tano sawa na sare ilizoambulia ndani ya ligi.

Masau Bwire, Ofisa Habari wa Ruu Shooting ameweka wazi kuwa watapambana kupata ushindi kwenye mechi ngumu.

Previous articleYANGA 1-0 US MONASTIR
Next articleYANGA YATINGA ROBO FAINALI,YALIPA KISASI