Home Sports YANGA YATINGA ROBO FAINALI,YALIPA KISASI

YANGA YATINGA ROBO FAINALI,YALIPA KISASI

YANGA imetinga hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho kwa ushindi wa mabao 2-0 US Monastir ya Tunisia.

Hiki ni kisasi ambacho wamekilipa Yanga chini ya Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi kwa kuwa mchezo waliokutana nao ugenini nao walitunguliwa mabao 0-2.

Ngoma ilikuwa ni mwendo wa mojamoja kila kipindi ambapo Kenned Musonda alianza kupachika bao dakika ya 33.

Kipindi cha pili ni Fiston Mayele alipachika bao dakika ya 78 na kufanya zawadi ya mama kuwa ni m 10 kwa mabao mawili na wanaongoza kundi D.

Previous articleMWEDNO WA RUVU NI WA KINYONGA
Next articleMWARABU KAFA NANI ANAFUATA? HUYU HAPA MPINZANI WA SIMBA