Home Uncategorized KMC MAJANGA, MTIBWA IHEFU ZAPETA

KMC MAJANGA, MTIBWA IHEFU ZAPETA

WAKIWA Uwanja wa Manungu, Mtibwa Sugar wamekata tiketi ya kutinga hatua ya robo fainali ya Kombe la Azam Sports Federation.

Ni ushindi wa bao 1-0 ambao walipata huku mtupiaji akiwa ni David Kameta, ‘Duchu’ dakika ya 45 kwa mkwaju wa penalti uliowandoa mazima KMC kwenye mashindano.

KMC hawana bahati pia kwenye mashindano haya kwa kuwa hawajawa kwenye mwendo bora ndani ya ligi pia.

Mbali na KMC kufungashiwa virago pia Pan African nayo imesepa kwenye mashindano haya baada ya kupoteza dhidi ya Ihefu.
Baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Highland Estate, Mbeya ulisoma Ihefu 2-0 Pan African

Mechi hizo zilichezwa Machi 4,2023 na leo Kagera Sugar itamenyana na Mbeya City huku Azam FC ikimenyana na Mapinduzi.

Previous articleNAMUNGO WAIVUTIA KASI TANZANIA PRISONS
Next articleHUYU HAPA KOCHA MPYA STARS