Home Sports VIGONGO VYA AZAM FC MACHI NI HIVI HAPA

VIGONGO VYA AZAM FC MACHI NI HIVI HAPA

MATAJIRI wa Dar Azam FC ndani ya Machi wana vigongo vikali vya moto viwili pekee ambavyo ni dakika 180.

Timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, Kali Ongala kete yake moja ni Kombe la Azam Sports na nyingine moja ni ya ligi.

Itakuwa nyumbani Machi 5, Jumapili kusaka ushindi dhidi ya Mapinduzi ikiwa ni hatua ya 16 bora.

Kisha itasepa na kuibukia Mbeya Machi 13 itakuwa na kigongo cha kufunga Machi dhidi ya Ihefu.

Huu mchezo dhidi ya Ihefu Uwanja wa Highland Estate utakuwa ni wa Ligi Kuu Bara na utachezwa saa 10:00 na ule wa Mapinduzi utachezwa saa 1:00 Azam Complex.

Tayari timu hiyo ipo kwenye maandalizi kwa ajili ya mchezo wake ujao ambao ni wa Shirikisho ikishinda hapo inakwenda kutinga hatua ya robo fainali.

Previous articleUMAKINI UNAHITAJIKA KUFIKIA MALENGO
Next articleBARCELONA NA MAAJABU YA MPIRA WAKISHINDA DHIDI YA REAL MADRID