Home International BARCELONA NA MAAJABU YA MPIRA WAKISHINDA DHIDI YA REAL MADRID

BARCELONA NA MAAJABU YA MPIRA WAKISHINDA DHIDI YA REAL MADRID

LICHA ya Real Madrid kuwa bora kwenye kila idara dhidi ya Barcelona kwenye mchezo wao wa El Clasico ngoma iliwazidia na kupoteza mchezo huo.

Baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Santiago Bernabeu ulisoma Real Madrid 0-1 Barcelona ambao walikuwa ugenini bado kete moja watakayokuwa nyumbani.

Ni Eder Militao alijifunga dakika ya 26 kwenye harakati za kuokoa hatari na mwisho ngoma ikazama kambani ikadumu mpaka mwisho wa mchezo.

Rekodi zinaonyesha kuwa ni Real Madrid walifanya mashambulizi mengi ambapo walipiga jumla ya mashuti 13 huku Barcelona wakipiga mashuti manne.

Ile ajabu ya mpira inaonesha kwamba Real Madrid hakuna shuti ambalo lililenga lango kwenye dabi hiyo huku Barcelona ikiwa ni mashuti mawili.

Ukitazama upande wa umiliki wa mpira Real wao walikuwa na asilimia 65 huku Barcelona ikiwa ni 35 hata kona ni 11 Real walipiga wapinzani wao mbili pekee.

Previous articleVIGONGO VYA AZAM FC MACHI NI HIVI HAPA
Next articleSAA 3 NZITO ZA KESI YA FEI V YANGA,SIMBA YAITANGULIA