Home Sports UMAKINI UNAHITAJIKA KUFIKIA MALENGO

UMAKINI UNAHITAJIKA KUFIKIA MALENGO

TUPO kwenye ulimwengu wenye ushindani mkubwa kwenye kila idara kuanzia Ligi Kuu Bara mpaka Kombe la Shirikishola Azam Sports hapa kila timu inahitaji ushindi.

Ipo wazi kwamba mashindano yamekuwa yanazidi kuwa imara kila wakati na timu shiriki zinafanya kweli kwenye kusaka ushindi hili linahitaji pongezi.

Wachezaji kwa sasa ni muda wao kuonyesha ule uwezo kwenye haya mashindano ambayo yanafuatiliwa na kila mmoja anajukumu kutimiza kazi yake.

Unaona kuna wachezaji wengine walikosa nafasi kwenye mechi za ligi na wapo ambao walikuwa wanashiriki mashindano ya kimataifa bado hawakupata nafasi ni muda wao kwenye haya mashindano.

Mechi ni chache kisha unafika hatua ya fainali na ukitwaa taji unakwenda kwenye mechi za kimataifa, nini tena wachezaji mnataka zaidi ya kupambana kwa hali na mali.

Kushinda kunaleta raha na hilo lipo wazi kwani wachezaji huwa wanafurahi na mashabiki nao wanakuwa kwenye kile kilele cha furaha pale wanaposhinda.

Basi ni muda wenu kufanya kweli lakini lazima mlindane wenyewe sio kwa kuwa ni kombe la kimataifa basi kila mchezaji apanie kufanya vizuri mpaka kumpa maumivu mchezaji mwingine.

Kama ilivyo kawaida kwenye makosa hapo ni pakufanyia maboresho wakati ujao ili kuwa imara na kila mmoja anatambua kwamba kinachowabeba wachezaji ni maandalizi.

Maandalizi mazuri yanahitajika kwenye kila hatua tuna amini itakuwa hivyo kwenye mechi zote.

Previous articleVIDEO: SAKATA LA FEI TOTO LAMUIBUA MAMA
Next articleVIGONGO VYA AZAM FC MACHI NI HIVI HAPA