Home Uncategorized DODOMA JIJI KUMALIZANA NA IHEFU

DODOMA JIJI KUMALIZANA NA IHEFU

UONGOZI wa  Dodoma Jiji  umeweka wazi kuwa baada ya kupoteza mchezo wao wa ligi dhidi ya  Mtibwa Sugar  hasira zao wanazihamishia kwa  Ihefu .

Kwenye mchezo waliokuwa Uwanja wa  Manungu  walipoteza kwa kufungwa mabao 2-1.

Leo Februari 24,2023 Dodoma Jiji wana kazi ya kusaka pointi tatu muhimu dhidi ya Ihefu ya Mbeya.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa saa 1:00 usiku kwa timu hizo uonyeshana ubabe wao.

Ofisa Habari wa  Dodoma Jiji, Moses Mpunga  amesema kuwa kushindwa kupata matokeo  mchezo uliopita hasira zinahamia kwenye mchezo dhidi ya Ihefu.

“Maandalizi yapo vizuri  tunamshukuru Mungu  na tupo tayari  kwa ajili  ya kupambana kwenye mchezo  huo ili kuweza kupata pointi tatu muhimu.

“Wapinzani wetu tunawaheshimu  tutaingia kwa tahadhari  kubwa maana kila timu   inahitaji  matokeo ili kuweze kujiweka kwenye  nafasi nzuri kwenye ligi kuu,”.

Kiingilio kwenye mchezo wa leo ni buku tu unawaona mastaa wote wa Ihefu na Dodoma Jiji.

Previous articleMANCHESTER UNITED WAINYOOSHA BARCELONA
Next articleAZAM FC KUMENYANA NA KMC AZAM COMPLEX