Home Sports AZAM FC KUMENYANA NA KMC AZAM COMPLEX

AZAM FC KUMENYANA NA KMC AZAM COMPLEX

BAADA ya kukamilisha kete yao dhidi ya Simba Uwanja wa Mkapa, kituo kinachofuata ni dhidi ya KMC.

Kwenye mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Mkapa ubao ulisoma Simba 1-1 Azam FC na kuwafanya wagawane pointi mojamoja.

KMC wao wametoka kupoteza mchezo wao uliopita dhidi ya Yanga uliochezwa Uwanja wa Mkapa.

Ubao ulisoma Yanga 1-0 KMC hivyo timu zote kwenye mechi zao zilizopita hazijaambulia pointi tatu.

Ni Uwanja wa Azam Complex mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Februari 25,2023.

Haseheem Ibwe, Ofisa Habari wa Azam FC amesema kuwa watapambana kupata pointi tatu dhidi ya KMC.

Christina Mwagala, Ofisa Habari wa KMC amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo na wanahitaji pointi tatu muhimu.

Previous articleDODOMA JIJI KUMALIZANA NA IHEFU
Next articleM-BET YAMWAGA MAMILIONI WASHINDI WAWILI, YAITAKIA KHERI SIMBA