Home Sports M-BET YAMWAGA MAMILIONI WASHINDI WAWILI, YAITAKIA KHERI SIMBA

M-BET YAMWAGA MAMILIONI WASHINDI WAWILI, YAITAKIA KHERI SIMBA

KAMPUNI ya mchezo ya kubashiri ya M-Bet Tanzania imewazawadia washindi wawili kila mmoja Sh175.3 millioni baada ya kubashiri kwa usahihi matokeo ya ligi mbalimbali duniani kupitia mchezo wa Perfect 12.

Washindi hao ni Mesharam Bakunda na Abdallah Segatwa ambao walizawadiwa fedha zao katika hafla fupi iliyofanyika makao makuu ya kampuni ya M-BET Tanzania jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya M-BET Tanzania, Allen Mushi amesema kuwa wanajisikia fahari kubwa kubadili maisha ya mashabiki hao wa soka ambao wote ni wafuasi wa Klabu ya Arsenal.

Mushi amesema kuwa washindi hao wawili wanaungana na wengine wengi katika nyumba ya mabingwa na kuwaomba mashabiki wa soka kujaribu bahati zao kwa kubashiri na kampuni yao.

“Mbali ya kubadili maisha ya washindi wetu kupitia kubashiri michezo, pia tunajisikia fahari kuchangia  asilimia 20 ya kodi ya ushindi ambayo inaigia moja kwa moja Serikalini. Sisi ni walipa kodi wazuri wa Serikali na tunachangia maendeleo,” amesema Mushi ambaye pia ameitakia Simba mafanikio mema katika mchezo wake na Vipers ya Uganda utakaochezwa kesho.

Kwa upande wake, Bakunda ambaye pia ni shabiki wa Yanga amesema kuwa hakuamini kushinda kiasi hicho cha fedha kwa kutumia Sh1, 000 tu.

 Amesema kuwa amekuwa akibashiri na M-BET mara kwa mara kwani ameshuhudia washindi kadhaa wakishinda fedha nyingi kupitia kampuni hiyo.

Naye Segatwa amesema kuwa hakukata tamaa katika safari yake ya kubashiri na mara kadhaa alikuwa anabashiri na kushinda fedha kidogo.

“Mimi mkulima, nitatumia fedha hizi kwa ajili ya kuendelza kilimo, kuboresha nyumba na kusomesha watoto wangu. Nimekuwa nikibashiri na kupata hela ndogo ndogo.

“Nilipopigiwa simu na kuambiwa kuwa nimeshinda zaidi ya milioni 100, sikuamini  na nilidhani ni ndoto,” amesema Segatwa.

Previous articleAZAM FC KUMENYANA NA KMC AZAM COMPLEX
Next articleMWAMBA CLATOUS CHAMA AWATULIZA SIMBA