Home Uncategorized YANGA YAKOMBA POINTI ZOTE ZA KMC

YANGA YAKOMBA POINTI ZOTE ZA KMC

HUKU kikosi cha Yanga kikiwa na nyota kadhaa ambao hawakuanza kikosi cha kwanza mchezo wa kimataifa dhidi ya TP Mazembe wamesepa na pointi tatu zote za KMC.

Kazi kubwa imemalizwa ndani ya dakika 40 za mwanzo ambapo bao lilipachikwa na Clement Mzize dakika ya 38 na kuipa pointi tatu Yanga.

Uimara wa ukuta wa timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi uliwapa tabu nyota wa KMC ikiwa ni pamoja na Matheo Athony kupata bao.

Ni Bacca na Bakari Mwamnyeto hawa walikuwa vizuizi huku kwa upande wa pembeni kukiwa na Kibwana Shomari.

KMC haijakusanya pointi dhidi ya Yanga mechi zote mbili na kichapo chake ni mwendo wa mojamoja.

Yanga inafikisha pointi 62 nafasi ya kwanza kwenye msimamo.

Previous articleRUVU SHOOTING INAPAMBANA KUREJEA KWENYE UBORA
Next articleMUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTI XTRA