Home Uncategorized MUDA BADO GARI HALIJAWAKA

MUDA BADO GARI HALIJAWAKA

MSIMU wake wa kwanza akiwa na Yanga baada ya kusajiliwa kwenye dirisha dogo akiwa ni mchezaji huru.

Kiungo Muadhathir Yahaya ameweka wazi kuwa bado hajafikia kwenye uwezo anaofikiria licha ya kupata nafasi za kucheza kwenye mechi za ushindani.

Nyota huyo ameingia jumlajumla kikosi cha kwanza cha Yanga kwenye eneo la kiungo mkabaji akionesha makeke yake kwenye mechi za ushindani.

Wakati Yanga ikiitungua mabao 3-1 TP Mazembe bao moja Muda alipachika nyavuni dakika ya 10 akitumia pasi ya Kennedy Musonda raia wa Zambia ambaye alifunga bao dakika ya 6.

Lile la tatu ni mali ya Tuisila Kisinda ambaye alipachika bao hilo dakika ya 90 akitumia pasi ya Fiston Mayele.

“Bado kazi inaendelea na ukweli ni kwamba kazi kubwa itafanyika kwa ajili ya kupata matokeo, bado sijafikia kile kiwango ambacho ninafikiria na tutazidi kuendelea kupambana kufanya vizuri,”.

Previous articleHAALAND THAMANI YAKE EURO BILIONI 1
Next articleSIMBA NA AZAM FC KITAWAKA,HAWA WATAKOSEKANA KWA MKAPA