Home Sports SIMBA NA AZAM FC KITAWAKA,HAWA WATAKOSEKANA KWA MKAPA

SIMBA NA AZAM FC KITAWAKA,HAWA WATAKOSEKANA KWA MKAPA

KAZI kubwa inatarajiwa kufanyika leo Uwanja wa Mkapa kwa Dabi ya Mzizima kati ya Simba v Azam FC unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.

Unakuwa ni mchezo wa pili kwa wababe hawa kukutana baada ya ule uliopita wa mzunguko wa kwanza ubao kusoma Azam FC 1-0 Simba na kuwafanya Simba kuyeyusha pointi tatu muhimu.

Kocha Mkuu wa Simba, Roberto Oliviera amesema kuwa wanatambua mchezo huo utakuwa mgumu lakini watapambana kupata ushindi.

“Haitakuwa kazi rahisi katika mchezo wetu ukizingatia kwamba tumetoka kupoteza katika mchezo tuliocheza dhidi ya Raja Casablanca na sasa tunajipanga kwa ajili ya mchezo wetu muhimu.

“Ninapenda kuona namna ambavyo wachezaji wanacheza, uwezo mkubwa na vipaji vipo hivyo tutaingia kwa mpango mzuri wa kutafuta pointi tatu na kila kitu kitakuwa sawa mashabiki waendelee kuwa pamoja nasi,” amesema Oliviera.

Ofisa Habari wa Azam FC, Hasheem Ibwe amesema kuwa wanatambua ni Dabi ya Mzizima ambayo itakuwa ngumu ila wapo tayari.

“Kukutana na Simba ikiwa imetoka kupoteza dhidi ya Raja Casablanca ni faida kwetu na hasara pia kwa kuwa wao wataingia na hasira za kimataifa tutapambana kupata matokeo mazuri,”.

Nyota wa Azam FC, Sospeter Bajana amesema kuwa wanatambua uimara wa wapinzani wao na tahadhari zote watachukua.

“Tunaingia kwa tahadhari kubwa kwa ajili ya mechi hiyo na tupo tayari kwa ajili ya mechi zijazo na tunachohitaji ni kupata pointi tatu muhimu,” amesema Bajana.

Watakaosekana kwa upande wa Simba ni Agustino Okra ambaye atakuwa nje kwa muda wa wiki nne kutokana na kutokuwa fiti Malickou Ndoye ni Kwa upande wa Azam FC anatumikia adhabu ya kadi nyekundu aliipata kadi nyekundu dhidi ya Dodoma Jiji.

Previous articleMUDA BADO GARI HALIJAWAKA
Next articleVIDEO:ISHU YA GARI LA SIMBA KURUDI KINYUMENYUME IPO HIVI