Home Uncategorized SIMBA WANA IMANI YA KUPATA USHINDI DHIDI YA AZAM FC

SIMBA WANA IMANI YA KUPATA USHINDI DHIDI YA AZAM FC

ROBERTO Oliveira, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa wamekuwa na matokeo mazuri kwenye mechi za hivi karibuni kwenye ligi jambo linalowapa imani ya kupata matokeo dhidi ya Azam FC.

Simba wamekuwa hawana bahati kwa kuwa mchezo uliopita wametoka kupoteza kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kunyooshwa mabao 3-0 dhidi ya Raja Casablanca.

Katika mchezo wao uliopita wa mzunguko wa kwanza dhidi ya Azam FC, Simba ilitunguliwa bao 1-0 na kuwafanya wayeyushe pointi tatu mazima.

Oliveira amesema:”Tunatambua ni mchezo mgumu na tumekuwa na matokeo mazuri kwenye mechi za ligi hivyo tutaingia kwa hesabu za kusaka ushindi wachezaji wapo tayari,”.

Kali Ongala, Kocha Mkuu wa Azam FC amesema wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo na watapambana kupata ushindi.

Previous articleMwezi Februari Umekuwa Mtamu Sana kwa Washindi Hawa wa Meridianbet
Next articleVIDEO:NABI AFICHUA SIRI KUWAFUNGA TP MAZEMBE