Home Uncategorized SIMBA NDANI YA ARDHI YA TANZANIA

SIMBA NDANI YA ARDHI YA TANZANIA

MSAFARA wa Simba umewasili salama Dar ukitokea nchini Guinea ulipokuwa kwa ajili ya kazi ya kuiwakilisha nchi kimataifa.

Chini ya Kocha Mkuu, Roberto Oliveira kikosi hicho kilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Horoya kwenye mchezo wa kwanza hatua ya makundi na kuyeyusha pointi tatu.

Kazi kubwa kwa sasa ni kuelekea mchezo wao ujao ambao utakuwa wa pili kwenye kundi C dhidi ya Raja Casablanca.

Simba ipo kundi C ambapo timu nyingine ni Vipers ya Uganda iliyopoteza mchezo wake wa kwanza pia mbele ya Raja ambao wanaongoza kundi wakiwa na pointi tatu tofauti ya mabao ya kufunga dhidi ya Horoya.

Miongoni mwa wachezaji ambao wapo kwenye msafara uliowasili salama ni Sadio anoute, Mzamiru Yassin, Mohamed Hussein, John Bocco na Clatous Chama.

Mchezo wao dhidi ya Raja unatarajiwa kuchezwa Februari 18 saa 1:00 usiku, Uwanja wa Mkapa.

Previous articleLIGI YA MABINGWA KITAWAKA PSG vs BAYERN MUNICH PATA ODDS BOMBA KUTOKA MERIDIANBET
Next articleNABI AWACHOMOA MASTAA YANGA, CHAMA,BALEKE WAKABIDHIWA WAARABU