Home Uncategorized KOCHA SINGIDA BIG STARS KUFANYIA KAZI MAKOSA

KOCHA SINGIDA BIG STARS KUFANYIA KAZI MAKOSA

KOCHA Mkuu wa Singida Big Stars Hans Pluijm amesema kuwa makosa ambayo wamefanya kwenye mchezo dhidi ya Ihefu watafanyia kazi kwa mechi zijazo.

Februari 12 2023 Singida Big Stars ilitoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1 dhidi ya Ihefu kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Highland Estate.

 Pluijm amesema kuwa walikuwa wanahitaji pointi tatu kwenye mchezo huo jambo ambalo lilishindikana.

“Tulipambana kutafuta ushindi kwenye mchezo wetu lakini mwisho haikuwa hivyo na tulikuwa tunahitaji ushindi hivyo ni muda wa kujipanga kwa mechi zijazo.

“Wakati mwingine huwa kunakuwa na presha kubwa kwenye mechi lakini ni muhimu kuwa watulivu na kuwaambia wachezaji wacheze mechi zao.

“Kila muda unaona tunakuwa na mechi ambazo zinatuhusu wachezaji wapo wengi na wanafanya hivyo tunazidi kujipanga kwa mechi zijazo kwenye makosa ambayo tumefanya,” amesema.

Ni Meddie Kagere alifunga kwa upande wa Singida Big Stars huku kwa upande wa Ihefu Yacouba Songne yeye alipachika bao lililoweka usawa kwenye mchezo huo.

 

Previous articleMSHINDI WA TZS 20M MERIDIANBET AELEZA MBINU ALIZOTUMIA
Next articleRAIS SAMIA ATANGAZA KUNUNUA KILA BAO YATAKAYOFUNGWA NA SIMBA NA YANGA KIMATAIFA