Home International YANGA HAWANA JAMBO DOGO WAANZA MAZOEZI

YANGA HAWANA JAMBO DOGO WAANZA MAZOEZI

WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye anga za kimataifa katika Kombe la Shirikisho Afrika, Yanga hawana jambo dogo baada ya kuanza mazoezi kwa ajili ya mchezo huo.

Msafara wa wachezaji 27 ulikwea pipa Februari 7 kwa ajili ya kuanza safari kuelekea Tunisia wakipitia Dubai ambapo kwenye msafara wao walikuwa wameongozana na madaktari wao pia.

Madaktari wa Yanga wanaingia kwenye orodha ya wale waliofanya kazi ya kuokoa maisha ya mgonjwa ndani ya ndege alipopatwa na tatizo walipokuwa wakielekea Dubai jambo ambalo linastahili pongezi na walikuwa wanatimiza majukumu yao.

Tayari msafara huo umewasili nchini Tunisia ambapo watacheza na US Monastri Februari 12 siku ya Jumapili mchezo ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa ikiwa ni hatua ya makundi.

Februari 8 waliwasili Tunisia na kuanza mazoezi mepesi kwa ajili ya kurejesha viungo kwenye usawa baada ya kuwa kwenye safari kwa muda.

Ally Kamwe Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa wapo tayari kwa mchezo huo.

“Tupo tayari kwa ajili ya mchezo wetu na tunawaomba mashabiki wazidi kutuombea dua ili tufanye kazi kwa usahihi inawezekana,”

Previous articleMWISHO WA MJADALA, MOROCCO INATOSHA AFCON 2025
Next articleSIMBA KAMILI KUIVAA HOROYA KIMATAIFA