Home Uncategorized SIMBA YAMTAMBULISHA MWAMBA HUYU

SIMBA YAMTAMBULISHA MWAMBA HUYU

ISMAEL Sawadogo kiungo mkabaji raia wa Burkina Faso ametambulishwa rasmi ndani ya kikosi cha Simba.

Ni raia wa Burkina Faso ameletwa duniani 1996 ana miaka 26.

Alikuwa anakipiga Klabu ya Difaa Hassani El Jadid

Anakuja kuchukua mikoba ya Victor Ackpan ambaye atatolewa kwa mikopo.

Ackpan raia wa Nigeria amekwama kufiti kikosi cha kwanza cha Simba kutokana na kuanza msimu akisumbuliwa na majeraha na hata aliporejea kwenye ubora wake bado hakuwa imara.

Juma Mgunda, kocha msaidizi wa Simba aliweka wazi kuwa nyota huyo atakuja kuwa imara taratibu kwenye kikosi hicho.

Kwa sasa Ackapn hayupo na timu nchini Dubai ambapo imeweka kambi kutokana na sababu zilizoelezwa kuwa anafuatilia masuala ya hati yake ya usafiri.

Anakuwa nyota wa pili kutambulishwa ndani ya kikosi cha Simba baada ya kuanza na Said Ntibanzokiza ambaye alikuwa anakipiga ndani ya Geita Gold.

Previous articleKAULI ya KWANZA ya MANDONGA BAADA ya USHINDI, AKANUSHA KUPIGWA ‘KO’ – ”MULIKUWA NA JAMBO LENU”..
Next articleWATATU KUIKOSA IHEFU KESHO