ARSENAL WAMOTO,WAIPOTEZA CITY KWA POINTI KIBAO

KIKOSI cha Arsenal kimewatungua mabao 4-2 Brighton kweye mchezo wa kuamkia Januari Mosi 2022 Soka.

Ni mabao ya Bukayo Saka dakika ya pili, Martin Odegaard dakika ya 39, Eddie Nketiah dakika ya 47 na Gabriel Martinelli dakika ya 71 hawa walifunga katika Uwanja wa Amex.

Paul Merson anasema nafasi ya Arsenal kuwa kilelei ndani ya Ligi Kuu Engaland  sio “babaisha”, huku Alan Smith akiamini kuwa kikosi hicho ni ‘kikongwe na chenye hekima’ kwa ajili ya kutwaa ubingwa.

Mabao ya Brighton yalifungwa na Kaoru Mitoma dakika ya 65 na Evan Ferguson dakika ya 77.

Baada ya wapinzani wao Manchester City na Newcastle kupoteza pointi mapema kwenye mkesha wa Mwaka Mpya, The Gunners waliwafunga Brighton 4-2 kwenye Uwanja wa Amex.

Arsenal wanafikisha pointi 43 tofauti ya pointi 7 na City iliyo nafasi ya pili na pointi 36.

Wakati bado kuna mechi 22  na msururu wa ratiba katika mwaka mpya ambao unaweza kufafanua matarajio yao ya ubingwa .

“Arsenal wanacheza vizuri sana, haikuwa ya kubahatisha,” Merson aliambia Sky Sports.