AZAM FC YAFUNGA MWAKA KIBABE

UBAO wa Uwanja wa Azam Compex baada ya dakika 90 ulisoma Azam FC 6-1 Mbeya City na kuwafanya matajiri hao kufunga mwaka kibabe.

ni Sopu alitupia kambani mabao mawili, Prince Dube, Keneth Muguna ,Nado na
Mkandala walitupia bao mojamoja.

Mchezo huo ulichezwa Uwanja wa Azam Complex ulikuwa ni wa kufungia mwaka 2022.

Bao la Meya City lilifungwa na Richardson Ng’ondya ambaye aliwapa bao la kufutia machozi mashabiki wake.

Azam FC inalipa machungu yakupoteza kwa kutunguliwa mabao 3-2 dhidi ya Yanga kwenye mchezo wao uliopita.