Home Sports WATATU WATEMWA NDANI YA AZAM FC

WATATU WATEMWA NDANI YA AZAM FC

KIKOSI cha Azam FC leo Desemba 31,2022 kitamenyana na beya City kikiwa kimeachana na nyota wake wawili jumlajumla.

Ni kipa namba mbili Ahmed Salula ambaye msimu huu hajapata nafasi ya kuanza kikosi cha kwanza pamoja na nyota Chilunda.

Wanafikisha idadi ya nyota watatu ambao wameachwa na Azam FC wakiungana na Ibrahim Ajibu ambaye anaibukia ndani ya Singida Big Stars.

Kwenye msimamo Azam FC ipo nafasi ya tatu baada ya kucheza mechi 18 za ligi ina pointi zake kibindoni 37 huku vinara wakiwa ni Yanga wenye pointi 47 baada ya kucheza mechi 18.

Kali Ongala, Kocha Mkuu wa Azam FC amesema kuwa wanatambua mechi za ligi ni ngumu na ushindani ni mkubwa hivyo watapambana kupata matokeo.

“Tunajua ushindani ni mkubwa na wapinzani wetu wanahitaji matokeo hivyo kila mechi tutakuwa na mpango mzuri kupata pointi tatu na wachezaji wapo tayari,”.

Azam FC inakutana na Mbeya City yenye pointi zake 21 kibindoni baada ya kucheza mechi 18.

Previous articleLIVERPOOL WASHINDA KWA ZAWADI YA MABAO
Next articleYANGA BILA FEI TOTO, KWA MIFUMO HII UNAPASUKA, SAIDO REKODI