Home Uncategorized SIMBA WANAHITAJI USHINDI KWENYE MECHI ZAO

SIMBA WANAHITAJI USHINDI KWENYE MECHI ZAO

JOHN Bocco nahodha wa Simba ameweka wazi kuwa malengo makubwa ya timu hiyo ni kupata matokeo kwenye mechi zote wanazocheza.

Mchezo ujao wa Simba ni dhidi ya Tanzania Prisons unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.

Mchezo wa mzunguko wa kwanza ubao wa Uwanja wa Sokoine Mbeya ulisoma Tanzania Prisons 0-1 Simba ambapo bao la ushindi lilifungwa na Jonas Mkude.

Mkude alitumia pasi ya mwamba Kibu Dennis ambaye alitoa pasi yake ya kwanza msimu wa 2022/23.

Bocco amesema:”Tunajua ushindani kwenye ligi ni mkubwa nasi tunahitaji kupata matokeo chanya kwenye kila mechi,”.

Previous articleMIDO AS VITA AFUNGUKA KUTUA YANGA
Next articleLIGI IMECHANGANYA, MECHI KALI ZA FUNGA MWAKA 2022 ZENYE ODDS KUBWA NA MACHAGUO KIBAO MERIDIANBET