Home Uncategorized JEMBE JIPYA SIMBA LAIBUKIA MWANZA

JEMBE JIPYA SIMBA LAIBUKIA MWANZA

BAADA ya kujiunga na kikosi cha Simba na kutambulishwa rasmi leo Desemba 24,2022 kiungo Said Ntibanzokiza ameibukia Mwanza.

Nyota huyo ambaye alikuwa ndani ya kikosi cha Geita Gold mwanzoni mwa msimu wa 2022/23 atakuwa na uzi wa Simba inayonolewa na Kocha Mkuu Juma Mgunda.

Kikosi cha Simba kwa sasa kipo Mwanza ikiwa ni kwa ajili ya maandalizi ya mwisho kuikabili KMC kwenye mchezo wa ligi unaotarajiwa kuchezwa Desemba 26,2022.

Ni dili la mwaka mmoja na nusu amepewa ndani ya kikosi cha Simba.

Kiungo huyo ana pasi sita za mabao akiwa ametupia mabao manne ndani ya Geita Gold.

Previous articleISHU YA FEISAL YAZUIA GUMZO,TAMKO YANGA LATOLEWA
Next articleWAAMUZI UMAKINI UNAHITAJI KWENYE MAAMUZI