Home Uncategorized RATIBA YA LIGI KUU BARA

RATIBA YA LIGI KUU BARA

RUVU Shooting chini ya Kocha Mkuu, Mbwana Makata ina kibarua cha kusaka ushindi kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mtibwa Sugar.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Uhuru katika msako wa point tatu muhimu.

Mchezo uliopita Ruvu Shooting ilipoteza pointi tatu mbele ya Ihefu ambapo ilifungwa mabao 2-0 lile moja ni mali ya Obrey Chirwa na jingine Ruvu Shootin walijifunga kwenye harakati za kuokoa hatari.

Mbali na mchezo huo pia Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi itakabiliana na Coastal Union ya Tanga chini ya Joseph Lazaro.

Mchezo mwingine ni ule kati ya Namungo v Ihefu pale Uwanja wa Majaliwa.

Previous articleRASMI KOCHA COASTAL UNION ABWAGA MANYANGA
Next articlePATA UTAMU WA CARABAO CUP UKIWA NA ODDS BOMBA KUTOKA MERIDIANBET