Home Uncategorized MKUDE NDANI YA BUKOBA KAZI IPO

MKUDE NDANI YA BUKOBA KAZI IPO

 LEGEND Jonas Mkude ni miongoni mwa nyota wa kikosi cha Simba ambao wapo kwenye msafara uliowea kambi Bukoba.

Kikosi cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Juma Mgunda kina kibarua cha kusaka pointi tatu dhidi ya Kagera Sugar, Uwanja wa Kaitaba.

Ikumbukwe kwamba Simba msimu wa 2021/22 ilinyooshwa bao 1-0 na Kagera Sugar katika mchezo uliochezwa Kaitaba kwa bao la Kiiza Diego ambaye alifunga akitokea benchi.

Pia alionyeshwa kadi mbili za njano zilizofanya akaonyeshwa kadi nyekundu kwenye mchezo huo ambao Simba walianza kupoteza dira ya kutetea ubingwa wao ambao ulisepa na Yanga.

Mbali na Mkude kiungo Clatous Chama, Pape Sakho, Jonas Mkude, Erasto Nyoni nao ni miongoni mwa wachezaji ambao wapo kwenye kikosi hicho

Previous articleCHAMA AMVUTA STARAIKA MZAMBIA SIMBA SC,YANGA YAMBAKISHA JOB
Next articleRASMI KOCHA COASTAL UNION ABWAGA MANYANGA