Home International NI ARGENTINA YATWAA KOMBE LA DUNIA, GONZALO SHUJAA

NI ARGENTINA YATWAA KOMBE LA DUNIA, GONZALO SHUJAA

TIMU ya Taifa ya Argentina inayoongozwa na Lionel Messi imetwaa taji la Kombe la Dunia Qatar 2022 kwa ushindi wa penalti 4=2 dhidi ya Ufaransa ya Kylian Mbappe.

Ufarasa walikuwa ni mabingwa watetezi wamevuliwa taji lao leo kwenye mchezo wakukata na shoka ambao umeshuhusia hat trick kutoka kwa Mbape.

Mara ya mwisho Argentina kutwaa taji hilo la Kombe la Dunia ilikuwa ni mwaka 1986 na leo kwenye mchezo bora wamesepa na taji hilo kwa ushindi wa penalti baada ya dakika 120 kumeguka kwa wababe hao kutoshana nguvu.

Kwenye fainali  ya kibabe Uwanja wa Lusail Iconic na inashuhudiwa hat trick kutoka kwa miguu ya kijana mdogo Kylian Mbappe dhidi ya Argentina.

Messi nahodha wa Argentina ametupia kambani mawili dakika ya 23 kwa mkwaju wa penalti na dakika ya 108 na bao lingine ni mali ya Di Maria ambaye alifunga bao dakika ya 26.

Mbappe kafunga dakika ya 80 kwa mkwaju wa penalti,81 na 118 kwa mkwaju wa penalti.

Messi mwenye miaka 35 hii ni fainali yake ya mwisho ya Kombe la Dunia ambapo mara ya ushindi huo alionekana akiwaaga mashabiki wake kwa kuwaambia asante.

Nyota Gonzalo Montiel ameweka rekodi yake kwa kuwa penalti yake ya mwisho aliyopiga na kuzama kambani imekuwa chachu ya ubingwa kwa timu yake ya Argentina.

Mashabiki 88,966 walikuwa mashuhuda wa mchezo wa leo uliokamilisha mbio za ubingwa wa kombe la dunia hivyo tuonane miaka minne ijayo.

Previous articleKIBU ACHEKA NA NYAVU, GEITA 0-5 SIMBA
Next articleKOMBE LA DUNIA NA TUZO BINAFSI WAMESEPA NAZO ARGENTINA