Home Sports KIBU ACHEKA NA NYAVU, GEITA 0-5 SIMBA

KIBU ACHEKA NA NYAVU, GEITA 0-5 SIMBA

MWAMBA Kibu Dennis leo Desemba 18,2022 amefungua akaunti yake ya mabao kwenye Ligi Kuu Bara.

Wakati ubao wa Uwanja wa CCM Kirumba ukisoma Geita Gold 0-5 Simba nyota huyo katupia bao moja dakika ya 89.

Bao hilo ametupia akitumia pasi ya kiungo namba moja wa pasi za mwisho ndani ya Simba Clatous Chama aliyetoa kwa mguu wake wa kulia akiwa nje ya 18.

Mabao mengine ya Simba yalifungwa na nahodha John Bocco ambaye alifungua pazi la mabao dakika ya 11 na bao la pili kufungwa ni mali ya Chama dakika ya 40.

Bao la tatu ni mali ya Pape Sakho aliyefunga mabao mawili dakika ya 47 na 75 kwenye mchezo ulioshuhudia kadi moja ya njano dakika ya 72 kwa kiungo Kelvin Nashon wa Geita Gold.

Previous articleMWAMUZI WA FAINALI HUYU HAPA
Next articleNI ARGENTINA YATWAA KOMBE LA DUNIA, GONZALO SHUJAA