Home International MWAMUZI WA FAINALI HUYU HAPA

MWAMUZI WA FAINALI HUYU HAPA

NI Szymon Marciniak raia wa Poland ameteuliwa kuwa mwamuzi wa kati kwenye mchezo wa fainali ya Kombe la Dunia leo Desemba 18,2022.

Ni Argentina dhidi ya Ufaransa ambao ni mabingwa watetezi wa Kombe la la Dunia.

Marciniak mwenye maiak 41, amekuwa mwamuzi wa FIFA tangu 2011 na fainali itakuwa mechi yake ya tatu huko Qatar, baada ya kuchezesha Ufaransa ushindi wa 2-1 dhidi ya Denmark katika hatua ya makundi na mtanange wa hatua ya 16 bora kati ya Argentina na Australia

Marciniak, ambaye atasaidiwa na Paweł Sokolnick na Tomasz Listkiewicz, alisema: “Kuwa mwamuzi katika fainali ya Kombe la Dunia … haiaminiki, kuwa mkweli. Ninajivunia sana mimi na timu yangu kwa sababu, bila shaka, sio Szymon Marciniak pekee, ni timu kubwa.”

Previous articleSABABU YA POLISI TANZANIA KUPIGWA 3-0 YANGA
Next articleKIBU ACHEKA NA NYAVU, GEITA 0-5 SIMBA