SportsKOMBE LA DUNIA NA TUZO BINAFSI WAMESEPA NAZO ARGENTINA Saleh3 years ago3 years ago01 mins TIMU ya Taifa ya Argentina imekabidhiwa taji lake leo baada ya kushinda Kombe la Dunia 2022 Qatar likiwa ni la tatu kwao. Ushindi wao wa penalti 4-2 dhidi ya Timu ya Taifa ya Ufaransa umepeleka furaha kwao huku maumivu yakiwa kwa wapinzani wao. Lionel Messi nahodha wa Argentina ametwaa tuzo ya mpira wa dhahabu huku nyota Mbappe wa Ufaransa yeye akitwaa kiatu cha ufungaji bora. Kwa upande wa tuzo ya kipa bora ipo mikononi mwa Emiliaono Martinez ambaye ni kipa wa Timu ya Taifa ya Argentina. Zilikuwa dakika 120 za kukata na shoka ambapo ngoma ilikamilikwa kwa sare ya kufungana mabao 3-3 na Mbappe kasepa na mpira baada ya kufunga hat trick. Post navigation Previous: NI ARGENTINA YATWAA KOMBE LA DUNIA, GONZALO SHUJAANext: CHAMA CHA WASIOONA TANZANIA WANEEMEKA NA MSAADA KUTOKA MERIDIANBET
Soccer Football - International Friendly - Spain v Brazil - Santiago Bernabeu, Madrid, Spain - March 26, 2024 Spain's Rodri scores their third goal from the penalty spot REUTERS/Violeta Santos Moura Je Fainali ya Kombe la Dunia 2026 Itakuwa Brazil vs Hispania? Saleh17 hours ago 0