Home International SAFARI YA ENGLAND IMEGOTA MWISHO, UFARANSA WAMO

SAFARI YA ENGLAND IMEGOTA MWISHO, UFARANSA WAMO

MABINGWA watetezi wa Kombe la Dunia Ufaransa wamekata tiketi ya kushiriki hatua ya nusu fainali baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya England.

Mabao ya Aurelien Tchouameni dakika ya 17 na lilela ushindi lilifungwa na Olivier Giroud dakika ya 78.

Ni nahodha wa Timu ya Taifa ya England, Harry Kane hakuamini macho yake baada ya kukosa penalti kwenye mchezo huo licha ya kwamba alifunga bao pekee kwenye mchezo huo dakika ya 54 na kuweka usawa kabla ya kufungwa bao lilioipa ushindi.

Kwenye mchezo huo wa hatua ya robo fainali ni timu zote zilikuwa zinapewa nafasi ya kutinga hatua ya nusu fainali kutokana na uborawa timu hizo pamoja na mbinu.

Sasa mabingwa hao watetezi watakutana na Morocco kutoka Afrika ambao walipata ushindi mbele ya Timu ya Taifa ya Ureno..

Kane amesema kuwa alifanya jitihada kusaka ushindi lakini ilishindikana na alikuwa anahitaji kufunga bahati haikuwa kwake.

“Nitawajibika katika hili, inaniumiza na inaumiza hasa ukizingatia kwamba tulikuwa na nafasi ya kushinda, penalti ya kwanza nilipiga vizuri kama ambavyo nilifikiria lakini penalti ya pili ilikuwa tofauti na vile ambavyo nilifikiria,”.

Previous articleVIDEO:SABABU ZA CEO BARBARA KUBWAGA MANYANGA/SIMBA KUTIKISIKA
Next articleGSM YAMALIZANA NA KIUNGO FUNDI, MAMBO MAWILI YAMUONDOA BARBARA SIMBA