Home Uncategorized ARGENTINA YA LIONEL MESSI YATINGA NUSU FAINALI KOMBE LA DUNIA

ARGENTINA YA LIONEL MESSI YATINGA NUSU FAINALI KOMBE LA DUNIA

MWAMBA Emiliano Martinez kipa wa Timu ya Taifa ya Argentina aliokoa penalti mbili kwenye mchezo wa hatua ya robo fainali.

Ni ile iliyopigwa na beki kitasa wa Timu ya Taifa ya Uswisi Virgil van Dijk na Berghuis, jambo lililowapa mlima mzito kuweza kutusua kwenye hatua hiyo.

Argentina ya Lionel Messi inatinga hatua ya nusu fainali kwa ushindi wa jumla ya penalti 4-3 baada ya dakika 120 kumeguka ngoma kuwa Uholanzi 2-2 Argentina.

Timu hiyo itakutana na Timu ya Taifa ya Croatia iliyoshinda mbele ya Timu ya Taifa ya Brazil kwenye hatua ya robo fainali.

Previous articleMSHINDI WA PROMOSHENI YA BETI NA KITOCHI MERIDIANBET
Next articleAZAM FC YAISHUSHIA KICHAPO MALIMALO