Home Uncategorized AZAM FC YAISHUSHIA KICHAPO MALIMALO

AZAM FC YAISHUSHIA KICHAPO MALIMALO

MCHEZO wa Raundi ya Pili, Azam Sports Federation, Desemba 9,2022 ikiwa ni siku ya kumbukizi ya miaka 61 ya Uhuru wa Tanzania ni mabao 9, Azam FC walipata.

Baada ya dakika 90, ubao wa Uwanja wa Azam Complex ulisoma Azam FC 9-0 Malimao FC.

Ilikuwa mwendo wamojamoja kwa watupiaji wa Azam FC ikiwa ni pamoja na Sospeter Bajana, Idd Chilunda, Muguna , Kipre Jr, Bin Zayd ,Kachwele na Chiwalanga.

Mr Hatrick, Abdul Suleiman, ‘Sopu’ yeye alitupia kambani bao mbili kwenye mchezo huo.

Kwa mechi ambazo zilichezwa Desemba 9,2022 huu ni mchezo wa kwanza ambao umekusanya mabao mengi ndani ya dakika 90.

Mchezo wa pili ni ule uliokusanya mabao sita uliwakutanisha Mbeya City v Stand FC, Uwanja wa Sokoine.

Kwenye mchezo huu ubao ulisomaMbeya City 5-1 Stand FC.

Previous articleARGENTINA YA LIONEL MESSI YATINGA NUSU FAINALI KOMBE LA DUNIA
Next articleISHU YA KIUNGO MGANDA KUGOMEA MKATABA YANGA IPO HIVI