ULIMWENGU wa mpira umeshuhudia maajabu leo baada ya timu ya taifa ya Morocco kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya timu ya taifa ya Ubegiji.
Ngoma ilikuwa nzito kuamini kwamba Morocco ingeibuka na ushindi kwenye mchezo huo ambao ulikuwa na ushindani mkubwa lakini maajabu ya mpira yamekamilika.
Ni mabao ya Abdelhamid Sabri dakika ya 73 na lile la pili lilipachikwa na Zakaria Aboukhal dakika ya 90+2.
Kwenye kundi F Morocco wanaongoza kundi wakiwa na pointi 4 na Ubelgiji ni nafasi ya pili a pointi tatu.
Pia kwenye mchezo wa leo ni mashuti 10 kila timu ilipiga huku Ubelgiji mashuti manne yakilenga lango na mashuti matatu yakilenga lango kwa Morocco.
Team Canada forward Jonathan David (#7) watches as his shot is saved by the Iceland goalkeeper during an international friendly match between Canada and Iceland at BMO Field in Toronto, Ontario, Canada, on March 28, 2026. (Photo by Indrawan Kumala/NurPhoto) (Photo by Indrawan Kumala / NurPhoto via AFP)