Home Uncategorized MSAFARA WA SIMBA NDANI YA ANGOLA

MSAFARA WA SIMBA NDANI YA ANGOLA

MSAFARA  wa wachezaji wa Simba pamoja na benchi la ufundi umewasili salama nchini Angola leo Oktoba 8,2022 kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya de Agosto.

 

Ni jumla ya wachezaji 24 ambao walikuwa kwenye msafara huo miongoni mwao ni pamoja na Aishi Manula, Ally Salim na Beno Kakolanya kwa upande wa makipa.

Viungo ni Clatous Chama, Pape Sakho, kiraka Erasto Nyoni, Mzamiru Yassin na Jonas Mkude.

Leo watafanya maandalizi ya mwisho kwa ajili ya mchezo wao wa kesho dhidi ya de Agosto nchini Angola.

Previous articleKIKOSI CHA YANGA DHIDI YA AL HILAL HIKI HAPA
Next articleYANGA YATOSHANA NGUVU NA AL HILAL KWA MKAPA