Home International ARSENAL WAPO JUU KILA KONA

ARSENAL WAPO JUU KILA KONA

KILA kona wapo juu hawa Arsenal wakiwa ni namba moja ukiweka kando Ligi Kuu England hata kwenye Kundi A katika Europa League ni namba moja.

Ushindi wa mabao 3-0 walioupata dhidi ya Bodo/Glimt unawafanya wawe hapo nafasi ya kwanza kwenye mchezo uliochezwa usiku wa kuamkia leo.

Ni mabao ya Eddie Nketiah dakika ya 23, Rob Holding dakika ya 27 na Fabio Vieira dakika 84 Uwanja wa Emirates.

Pointi 6 wanafikisha Arsenal huku Bodo/Glim ambao walipiga mashuti 8 na manne yakalenga lango wao wapo nafasi ya pili na pointi 4 baada ya kucheza mechi tatu.

Arsenal wao wamecheza mechi mbili pointi sita kibindoni kwenye kundi A.

Previous articleMECHI ZA USHINDI KWENYE MERIDIANBET WIKI HII
Next articleHII HAPA ORODHA YA MASTAA 25 WA AZAM FC KIMATAIFA