MUHIMU KWA WAAMUZI KUSIMAMIA SHERIA

    WAAMUZI ni sehemu muhimu kwenye mchezo hasa kutokana na kusimamia sheria 17 za mpira ambao unafuatiliwa na watu wengi duniani.

    Ipo wazi kuwa Ligi Kuu Tanzania Bara imekuwa kwenye ushindani mkubwa na kila siku hatua moja inapigwa kuyafuata matokeo.

    Kwa waamuzi wale ambao wamekuwa wakishindwa kutafsiri sheria za mpira ni muhimu kujifunza kupitia makossa ili wakati ujao wazidi kuwa imara zaidi.

    Kuna mapambano ambayo yamekuwa yakishindwa kwenda sawa kutokana na waamuzi kushindwa kusimamia sheria hizo kwa usawa.

    Makosa yapo kwa wachezaji na waamuzi pia lakini isiwe kwa kurudia mara kwa mara hasa kwa wakati huu ambao timu ikikosa pointi hata moja inaachwa kabisa kwenye mwendo.

    Wachezaji nao wanajukumu la kuongeza kazi ya kuwa makini kwenye mechi ambazo wanacheza hilo litawafanya wawapunguzie makosa waamuzi.

    Kwenye mechi ambazo zimepita inaonekana kuna maamuzi ambayo yalikuwa yakiwaumiza upande fulani na upande mwingine ambao unapata matokeo kufurahia.

    Suala la kupelekana kwenye kamati ya maamuzi hili lisiwe kwa waamuzi kwa kuwa wana muda wa kufanya mazungumzo wakiwa uwanjani .

    Hilo litawafanya wazidi kupata kile kilicho bora na kwa namna soka linavyozidi kukua umakini wao utawapa thamani na kuwa bora kwenye kazi yao.

    Kila kitu kinawezekana ni suala la muda kwenye kusubiri matokeo mazuri na hilo linasubiriwa kwenye mechi zote za ushindani.

    Sheria ni ngumu na hata nje nao wamekuwa wakishindwa kwenda nazo kutokana na kasi jambo ambalo limefanya teknolojia ya VAR kuletwa.

    Lakini licha ya uwepo wa hiyo bado makosa hayaishi yanaonekana.

    Previous articleVIDEO: UWEZO WA MGUNDA USIBEZWE ATAIFIKISHA NUSU FAINALI
    Next articleIHEFU YAAMBULIA POINTI LIGI KUU BARA