Home Sports IHEFU YAAMBULIA POINTI LIGI KUU BARA

IHEFU YAAMBULIA POINTI LIGI KUU BARA

IKIWA Uwanja wa Highland Estate, leo Oktoba 4,2022 Klabu ya Ihefu imekusanya pointi moja kwa mara ya kwanza msimu wa 2022/23.

Ikumbukwe kwamba Ihefu inayonolewa na Kocha Mkuu, Juma Mwambusi kwenye mechi nne mfululizo ilipoteza mechi zake na mchezo wake wa mwisho kabla ya leo ilifungwa mabao 2-1 KMC.

Sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Tanzania Prisons imewapa pointi moja ikiwa nyumbani.

Ni bao la Jaffary Kibaya dakika ya 55 ambaye alifunga liliwekwa usawa na Ismail Mgunda dakika ya 81.

Prisons yenye David Mlipili mchezo wao uliopita walitoka kushinda bao 1-0 dhidi ya Azam FC.

Mbali na mchezo huo pia Geita Gold imeshinda mabao 2-1 Polisi Tanzania kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

Kwa Polisi Tanzania ni bao la Kapona dakika ya 66 huku yale ya Geita Gold yakifungwa na George Mpole dakika ya 45+1 na Edmond dkika ya 82.

Mpole ni mzawa ambaye anatetea kiatu chake cha ufungaji bora, alifunga mabao 17 msimu wa 2021/22.

Previous articleMUHIMU KWA WAAMUZI KUSIMAMIA SHERIA
Next articleKOCHA MPYA SIMBA QUEENS ATAJA KILICHOMLETA BONGO